Uongozi wa halmashauri ya wilaya ya kalambo mkoani Rukwa umetoa misaada ya vitu mbalimbali kwa watu waliokuwa wamethirika na maafa ya mvua ilionyesha march 2019 katika kata ya lyowa na kusabisha zaidi ya watu120 kukosa makazi na huku ukisisitiza zaidi wananchi kujenga nyumba bora pamoja na kupanda miti kwa kila kaya kwa lengola kuondoka na adha ya kujirudia kwa matukio hayo.
Kata ya lyowa ni miuongoni mwa kata wilayani humo ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto kubwa ya mvua kuharibu makazi ya wananchi kila mwaka kutokana na maeneo hayo kuwa na ukosefu wa miti ya kutosha na huku mwaka 2019 zaidi ya watu 120 wakidaiwa kukosa makazi na hivyo kupelekea uongozi wa halmashauri hiyo kutoa misaada kwa watu waliokuwa wameathirika na maafa hayo.
Awali akikabithi misaada hiyo makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Legius Boimanda alisema wataendelea kutoa misaada kulingana nafedha zinavyopatikana na kuwasihi wananchi kuendelea kujenga nyumba bora na nimara kwakushirikana na wataalamu wa halmashauri husika.
Alisema misaada iliotolewa ni kutokana na michango ya watu mbalimbali kutoka kata ya Lyowa na Matai na kuwa watu 50 wamepatiwa fedha na vyakula na kusema wataendelea kutoa misaada kulingana na fedha zivyopatikana kutoka kwa wadau.
Alisema kila mwaka eneo hilo limekuwa nikikabiliwa na changamoto kubwa ya nyumba kuboka kutoka na maeneo hayo kuwa na ukosefu wa miti ya kutosha .
‘’ndugu wananchi ningewaomba mpande miti kwa wingi ili tuondokane na adha ya kuboka kwa nyumba zetu na pia ni vizuri kama kila mtu akijenga nyumba kwa kuzingatia kanuni bora za ujezi’’alisema Boimanda.
Baadhi ya wachunganji na mashehe waliupongeza uongozi wa halmashauri hiyo kwa jitihada hizo na kuwaombea kwa mungu kuendelea kuwa na moyo huo hata kwa watu wengine waliopata adha kama hiyo.
Hata hivyo kufuatia maafa hayo kutokea maeneo hayo mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura ,alisema kila mwananchi anawajibu wa kupanda miti mitano sambamba na kujenga nyumba bora na imara .
‘’niwakumbushe wananchi wangu kuwa kila mwananchi anawajibu wa kupanda miti kwa kila kaya ili kuondokana nadha hii ambayo imekuwa ikijitokeza kila wakati na kusababisha maafa’’alisema Binyura.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.