Serikali imetoa fedha billion 1.7 kwa ajili ya uchimbaji wa bwawa la maji katika kijiji cha Kalemasha wilayani Kalambo Mkoani Rukwa litakalohudumia watu 25000 kutoka vijiji vitano vya kata Mbuluma na kutatua changamoto ya muda mrefu ya maji iliyokuwa ikivikabili vijiji hivyo,
Kamati ya usalama ya wilaya ya kalambo imefanya ziara ya ukaguzi wa mradi huo leo Disemba 28/2022 ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo , ambapo mkuu wa wilaya hiyo Tano Mwela, amesema fedha hizo zimetolewa kwa ufadhili wa mfuko wa maji wa Taifa (Nation Water Fund )na kwamba awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa miundombinu ya maji itakayo hudumia wakazi wa vijiji 5 vya kata ya Mbuluma
‘’ujenzi wa miundombinu ya bwawa unafanywa na kampuni ya ujenzi ya Chelesi General Entreprises Limited kwa gharama za mkataba wa Tsh 1,770,686,098.83 ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika June 30/2022’’ alisema Mwela,
Mapema akiongea wakati wa ziara hiyo kaimu meneja wa Ruwasa wilayani humo Francis Mpunda , alisema mpaka sasa fedha shillingi milion 192,062,452.20 zimetumika na kusema mradi huo utaenda kuwawezesha wakazi wa vijiji hivyo kuondokana na adha ya maji ambayo ilikuwa ikiwakabili kwa muda mrefu
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.