Serikali kupitia wakala wa barabara za vijijini na mijini TARULA mkoani Rukwa imeanza utekelezaji wa ujeziwa mradi wa barabara ya lami yenye umbali wa km2 na kugharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mia nane katika mji mdogo halmashauri ya wilaya ya kalambo Matai na huku mkataba wake ikiwa ni miezi mitatu.
Mji wa matai ni miongoni mwa miji midogo inayokuwa kwa kasi kubwa mkoani Rukwa, licha ya hilo, mji huo umekuwa ukikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa barabara ya lami licha ya kuwa katikati ya makao makuu ya wilaya hiyo.
kwa kulina hilo serikali ilitoa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi million mianane kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami kwenye maeneo hayo.
Bensoni Ndunguru kaimu meneja wa Tarula wilayani humo amesema kiasi cha zaidi ya shilingi milioni mianane kitolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 2 na mkataba wake ikiwa ni miezi mitatu.
Mkuu wa wilaya hiyoJulieth Binyura amemtaka mkandasi kurakisha ujezi wa barabara hiyo na kumsihi kuweka sehemu za kupita magari wakati ujezi ukiendelea.
Akikagua ujezi wa barabara hiyo naibu waziri wa Nchi ofis Ya Rais Tamisem Josephat Kandege ametaka mkandarasi kushirikina na madiwani wakati wa ujezi wa barabara hiyo.
Hata hivyo Naibu waziri Kandege ametembelea na kukagua miradi mbalimbaliinayoendelea kutekelezwa wilayani humo ikiwemo hosptali ya wilaya pamoja na ujezi wa shule mpya ya wasichana ilipo katika kata ya lywa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.