...Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura akiwa na baadhi ya viongozi na maafisa wa Serikali katika zoezi la kuweka mpaka unaoonesha eneo la mita 60 kutoka ukingo wa ziwa Tanganyika ambalo halitakiwi kujengwa makazi katika kijiji cha Samazi kata ya Samazi.
Zoezi hilo ni moja ya shughuli zilizofanyika katika kuelekea kilele cha siku ya Mazingira duniani ambayo itaazimishwa siku ya Tar 05/06/2017, katika Mkoa wa Rukwa siku hiyo itaazamishwa katika Wilaya ya Kalambo.
Siku ya Mazingira Kitaifa itaadhimishwa katika Kijiji cha Butiama Mkoani Mara, Makamu wa Rais Mh. Samia Hassan Suluhu atakua mgeni rasmi ambapo kaulimbiu mwaka huu ni “Hifadhi mazingira, Muhimu kwa Tanzania ya viwanda”
Mkuu wa Wilaya akikagua mawe yanaoonesha mpaka wa mita 60 za ziwa Tanganyika katika kijiji cha Samazi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Eng. Saimon Ngagani (kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya Mh. Julieth Binyura wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Samazi juu ya nyumba zitakazo athirika na mpaka wa mita 60 wa ziwa Tanganyika.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.