Shirika la viwango Tanzania TBS limesema halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kuwapiga faini ya shilling million 20 wajasiliamali na wasindikaji watakao bainika kufoji nembo ya TBS pamoja na kuingiza sokoni bidhaa zisizokuwa na ubora.
Hayo yamebainishwa na kaimu meneja wa shirika la viwango Tanzania Tbs kanda ya Magharibi Rodney Alananga wakati akitoa elimu kwa wajasiliamali, wasindikaji na wamiliki wa viwanda na kufanyika katika ofisi za kata ya Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa,Ambapo aliwataka waandaji wa bidhaa kuzingatia weledi na viwango na ubora wakati wa uandaaji wa bidhaa kabla ya kuingizwa sokoni.
‘’Tbs inazo skimu mbalimbali za udhibiti ubora ikiwemo skimu ya alama ya ubora,mzalishaji ambaye bidhaa yake imethibitishwa ubora kwa kuzingatia kiwango cha kitaifa cha bidhaa husika hupewa leseni ya kutumia alama ya TBS katika bidhaa hiyo hivyo kwa mwaka 2024 mzalishaji yeyote ambaye atashindwa kuwa na alama hiyo kwenye bidhaa yake atazuiliwa bidhaa yake kuingizwa kwenye maonesho makubwa ikiwemo nane nane na saba saba. Alisema Rodney – Alananga.
Alisema alama ya TBS huwafanya wanunuzi kununua bidhaa bila wasiwasi wowote na kwa upande mwingine alama hiyo humlinda mzalishaji katika ushindani dhidi ya bidhaa hafifu na humwezesha kulihakikishia soko lake juu ya ubora.
Afisa afya wa Halmashauri ya Kalambo Queen Nyahenga, alisema miongoni mwa mikakati waliojiwekea kama halmashauri ni pamoja na kufanya kaguzi za mara kwa mara kwenye viwanda ili bidhaa ziweza kuzalishwa kwa viwango na kwa ubora na kuleta tija kwa watumiaji.
Kwa pande wake mmoja wa wamiliki wa viwanda akiwemo Kasimu malingu aliipongeza serikali kwa kutoa elimu ya uzalishaji wa bidhaa kwa ubora na kwamba wana uhakika wataweza kuzalisha bidhaa ambazo zitaleta ushindani kwenye masoko ya nje.
Hata hivyo Shirika la viwango Tanzania TBS lilianzishwa kwa sheria ya Bunge –sheria ya viwango No 3 ya mwaka 1975 iliyofanyiwa marekebisho na sheria Na 1 ya mwaka 1977 ambapo sheria hiyo ilifutwa
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.