utalii wa Nyuki (AP TOURLISM) Ambao Utampatia fursa Mtalii kujionea Shughuli za Ufugaji Nyuki Katika hifadhi ya Mazingira Asilia Kalambo ikiwa ni pamoja na kudungishwa Nyuki Mwilini Ili Kuchochea na Kuimarisha Kinga za Mwili kwa watalii ambao watakuwa wakitembelea hifadhi hiyo.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa utalii huo askari wa uhifadhi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Kalambo Daniel Dotto amesema katika kufanisha hilo serikali imeanzisha shamba maalum kwa ajili ya ufugaji nyuki na kutoa mizinga 500 yenye thamani ya shilingi million150 ambayo itawezesha watalii kujifunza namna bora ya ufugaji wa nyuki kisasa.
Amesema licha hilo mtalii ataweza kujionea mazingira halisi ya ufugaji nyuki na mazingira ikorojia ya msitu huo ikiwa ni pamoja na kutembelea maanguko ya maji ya mto Kalambo ambayo ni ya pili Afrika kwa urefu wa mita 235 kutoka maji yanapoanzia.
Kwa upande wake mhifadhi mkuu wa wakala wa hifadhi za misitu Tanzania TFS Braison Mkiwa amesema licha ya hilo uwepo wa utalii huo utawezesha kuongezeka kwa mapato ya serikali Pamoja na watalii wanaotembelea hifadhi hiyo ambao kwa sasa wamefikia elfu moja (1000) kwa mwaka na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo ili kujionea na kujifunza namna bora ya utengenezaji wa mizinga na ufugaji nyuki kisasa.
Hata hivyo uanzishwaji wa utalii huo ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha wawekezaji na watalii kutembelea vivutio vya ndani.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.