Wadau kutoka asasi zisizo kuwa za kiserikali zinazohusika na maswala ya ukatili wa kijinsia mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha baadhi ya wachungaji na watumishi wengine wa mungu kuto pima afya za waumini wao pindi wanapofunga ndoa na hivyo kupelekea kujitokeza migongano ya kifamilia kutokana na baadhi yao kukutwa na mambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kumekwepo na mamalamiko kutoka kwa wananchi mkoani Rukwa juu ya kujitokeza kwa migogoro ya kifamilia ambayo imekuwa ikisababishwa na baadhi ya wachungaji na watumishi wengine wa mungu kudaiwa kuto wapima wanandoa hao kabla ya kufungishwa ndoa .
Hali hiyo imepelekea wadau wanaohusika na maswala ya ukatili wa kijinsia na mila potofu kutoka Asasi ya Sumbawanga Community Development Achievement (SUCODA) kuingilia kati swala hilo kwa kutoa elimu kwa wachungaji,mashehe, watumishi wa serikali pamoja na watu wengine, lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa watu kupima kabla kufunga ndoa.
‘’tumeona ni vyema tukakaa na wachungaji ili kuwapatia mafunzo zaidi juu ya maswala ya ukatili wa kijinsia kwani kitendo cha mchungaji kufungisha ndoa bila kujua afya za wahusika, ni kitendo kibaya kwani kina sababisha kuongezeka kwa magonjwa ya ukimwi.’’alisema Mwazyunga.
Afisa maendeleo ya jamii wilayani humo Yasinta Nkyabonaki,amesema hali hiyo imekuwa ikisabisha kuongezeka kwa mambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na migogoro ya kifamilia.
Alphonsa Shirima afisa ustawi wa jamii wilayani humo,amesema wazazi wanawajibu wa kuwalea watoto wao katika mazingira bora ikiwemo kuwapatia mahitaji yote muhimu.
Kwa upande wake mwanasheria kutoka Asas isiyokuwa ya kiserikali ya SUCODA Jonas Chidowi, amesema ni kosa kisheria kwa wachungaji kuto pima afya za watu wanao funga ndoa.
‘’niwasihi wachungaji kujenga mazoea ya kupima afya za waumini wao hususani wale ambao wanaokuwa kwenye harakati za kuoa ama kuolewa kwa lengo la kupunguza kasi ya mambukizi ya ukimwi.alisema Chidowi.
Kwa upande wake mchungaji kutoka kanisa la Moravian katika wilaya ya Kalambo Tedysoni Nzalamwe, amesema changamoto kubwa imekuwa ikijitokeza kutokana na taarifa feki kutoka kwa wanandoa wenyewe ambazo zimekuwa zikisababisha wao kuingia kwenye migogoro.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.