Wahadhiri wandamizi kutoka chuo kikuu cha Dar Es Saalam of Technology (DIT) wamewataka wanafunzi mkoani Rukwa kuwekeza kwenye masomo ya sayansi kwa kuongeza bidii katika kusoma na kuyafanyia kazi wanayofundishwa na walimu darasani ili kufikia malengo yao ya badae ikiwemo kuwa wabobezi kwenye masomo hayo.
Wameyasema hayo wakati wa ziara ya kutoa mafunzo kwa wanafunzi wa shule za sekondari katika wilaya ya Kalambo na Sumbawanga mkoani Rukwa na kubainisha kuwa kwa sasa chuo hicho kinatoa kozi zote za masomo ya sayansi kuanzia ngazi ya Astashahada.
Mapema akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari Msanzi Wilayani Kalambo mmoja wa wahadhiri hao Dkt Asinta Manyele,amesema lengo la chuo hicho ni kupita kila shule ili kuhamasisha wanafunzi husani wa jinsia ya kike kuyapenda masomo ya Sanyasi kutokana na serikali kuboresha miondombinu ya maabara na vyumba vya madarasa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.