Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura amewasihi watumishi wilayani humo kuona umuhimu wa kuendelea kufanya mazoezi kama ilivyokuwa awali ili kuwawezesha kuimarisha miili yao ili isipatwe na magonjwa
Katika moja ya mitandao ya kijamii inayo jumuisha watu wote wanaofanya mazoezi wilayani humo, mkuu wa wilaya hiyo aliwasisitiza watumishi kuendelea na mazoezi kwa lengo la kuimarisha afya.
Aidha aliwasisitiza kumtegemea Mungu pamoja na kuchukua tahadhari wakati wa kufanya mazoezi hayo ambayo ni muhimu katika kuimarisha afya.
“wanamichezo Kalambo mcheze ili muimarishe afya. Mungu atawalinda hakuna atakayepata madhara. Tuendelee kuchukua tahadhari pia”. Alisisitiza Binyura.
Hivi karibuni kupitia mtandao huo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Msongela Palela aliwasisitiza watumishi kuendelea kufanya mazoezi kutokana na kuwa na umuhimu mkubwa
“Kama tumerudisha minada na sasa tunatafakari kurejesha ligi za Mpira hakuna sababu ya kuendelea kuzuia mazoezi. Mh Rais ameelekeza mazoezi yaendelee. Kwa muktadha huo naruhusu mazoezi yaendelee chamsingi tuzingatie maelekezo mbalimbali yanayotolewa”. Alisisitiza Msongela.
Hata hivyo Kulingana na ripoti ya shirika la afya duniani WHO, iliyochapishwa na The Citizen, takribani watu billioni 1.9 wanaugua ugonjwa wa sukari ama uzito wao kuongezeka maradufu. Shirika hilo pia lilipendekeza kufanya mazoezi kila mara kama njia bora ya kuimarisha afya.
Licha ya kwamba lishe ni muhimu katika kuongeza uzito, kwa watu wazima mazoezi pia ni muhimu. Ikumbukwe kwamba, kuongeza uzito kiafya kunahusisha kuongeza kiasi cha misuli zaidi ya kiasi cha mafuta. Kama utaongeza kiasi kikubwa cha mafuta utakuwa umetoka katika tatizo moja na kwenda kwenye tatizo lingine.
Mazoezi yanasaidia kuhakikisha unapoongeza uzito/mwili hautawaliwi na kuongezeka kwa mafuta mengi mwilini, kitu ambacho si kizuri kiafya.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.