Ziara ya mafunzo ya wahasibu themanini kutoka kanda nane za wakala wa huduma za misitu nchini-TFS- ya kuyatembelea maporomoko ya maji ya kalambo yaliyopo wilayani kalambo mkoa wa Rukwa imetoa elimu ya jinsi ya kuyatumia maporomoko hayo kwa faida za kiuchumi wa taifa.
Mhasibu mkuu wa TFS makao makuu Peter Mwakosya amesema maporomoko ya Kalambo yanayoshika nafasi ya pili kwa urefu barani Afrika hayajatumika kikamilifu kwa ajili ya manufaa ya taifa licha ya kuwa kivutio cha kupendeza kwa watalii wa ndani na nje
Amesema wakati umefika kwa serikali kushirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya utalii kuboresha miundo mbinu rafiki kwa ajili ya utalii ili kusaidia kukuza pato la taifa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii
Msaidizi mkuu wa meneja wa TFS kanda ya nyanda za juu kusini Innoncent lupembe amesema hivi sasa zimefanyika taratibu za kushirikiana na mamlaka husika za utalii nchini Zambia ili kwa pamoja kuyatumia maporomoko ya kalambo kwa faida .
Josephat Chezue meneja wa wakala wa hifadhi za misutu wilayani kalambo amesema mpaka sasa wanaendelea na ujenzi wa nyumba za kufikia wageni pamoja na ngazi za kupandia kutoka juu hadi chini na kuwataka watalii wa ndani na nje kuendelea kutembelea maeneo hayo
ziara ya mafunzo ya wahasibu kutoka kanda zote za TFS nchini inatarajiwa kuja na ufumbuzi sahihi wa matumizi sahihi yenye faida ya maporomoko ya Kalambo
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.