Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa siku 2 kwa wazazi kuhakikisha wanafunzi 932 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaripoti mara moja shuleni na kuanza masomo bila visingizio vyovyote na kuwaagiza watendaji wa kata na vijiji kuwakamata na kuwashitaki wazazi watakaoshindwa kuwapeleka watoto wao shule baada ya muda huo kupita katika Wilaya ya Kalambo.
Wangabo ametoa maagizo hayo katika kikao kazi kilicho jumuisha watendaji wa vijiji, kata na maafisa tarafa pamoja na wakuu wa idara wilayani Kalambo ambapo alisema wanafunzi 932 sawa na asilimia 31.7 waliotakiwa kuanza kidato cha kwanza hawajaripoti shuleni mpaka hivi sasa.
‘’Mimi natoa siku mbili kwa wazazi wote ambao wana watoto hawajaenda shule mpaka sasa hivi iwe ni wa darasa la kwanza, wawe ni “form one” (kidato cha kwanza) baada ya siku hizi tano wakamatwe wafikishwe mahakamani hatutaki mchezo kwenye elimu, huyu mtoto ukimchezea chezea hivi huyu huyu ndio atatusumbua, kwasababu akitoroka shule anakimbia yamesmshinda ndio huyo anakwenda mitaani, unadhani watoto wa mitaani wanatoka wapi si wameshindwa shule huku, si wazazi wameshindwa kuwalea, wakamatwe wazazi wanaoshindwa kuwalea watoto wao wafikishwe mahakamani, watendaji wa vijiji watendaji wa kata kamateni wazazi hao” Alisisitiza.
Mh. Wangabo alisema kuwa mkoa kufanya vibaya kwenye elimu kunachangiwa na kuchelewa kupeleka watoto shule na kuongeza kuwa endapo tathmini inafanyika kwa wale wanaofanya vibaya kwenye mitihani yao utagundua ni wale wanaochelewa kufika shule na kutahadharisha kuwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wapo katika kipindi cha mabadiliko kutoka kwenye ufundishwaji wa Kiswahili kwenda kwenye ufundishwaji wa kiingereza hivyo ni muhimu kwao kuwahi shuleni.
Awali afisa elimu sekondari wa wilaya ya Kalambo, Efraim Moses akisoma taarifa ya maendeleo ya elimu wilayani kwake alisema wanafunzi ambao hawajaripoti mpaka sasa ni 932, kati yao wavulana ni 430 na wasichana ni 502, baadhi ya washiriki wa kikao hicho wameeleza maoni yao.
‘’wilaya ina jumla ya shule za sekondari 19 zenye jumla ya wanafunzi 9,232 kati yao wavulana ni 5,084 na wasichana ni 4,148 .shule 15 zinamilikiwa na serikali na shule 4 zinamilikiwa na mtu binafsi’’alisema Mosesi.
Hata hivyo shule za serikali zina jumla ya wanafunzi 8,838 miongoni mwao hizo wavulana ni 4,886 na wasichana 3,952 .wanafunzi 8,115 ni kidato cha cha tano hadi cha sita {V-VI}.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.