Wananchi katika kijiji cha Kalambo kata ya Mpombwe Tarafa ya Matai wilayani kalambo mkoani Rukwa wamejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvamia eneo la hifadhi ya kalambo asilia na kufanya mauaji ya mnyama aina ya tembo kisha gawana nyama kinyume na utaratibu.
Akithibitha kutokea kwa tukio hilo afisa tarafa ya Matai Endrue Manyema Ngindo amesema watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kukamatwa na nyama ya tembo kufuatia msako mkali uliokuwa umefanyika kijijini hapo kufuatia kutokea kwa tukio hilo.
Amesema tukio hilo liligundulika baada ya baadhi ya wanakijiji kuonekana katika maeneo hayo wakigawana nyama na hivyo kupelekea uongozi wa kijiji na kata kutoa taarifa polisi ambao walifika mapema eneo la tukio na kisha kufanya msako mkali .
‘’watu watano tumewakamata wakiwa na nyara za serikali wa kwanza ni Lucas Mjanlwazira huyu tulimkamata na nyama ya tembo ,wapili ni Joseph mizyuka huyu tulimkamata pia na nyama ya tembo,watatu ni Mejani Sipanje huyu tulimkamata na nyama ya tembo,wa nne ni John Michael huyu pia tulimkamata na tembo na Jery Simtely huyu pia tulimkamata na mguu wa digidigi, vichwa viwili vya ndege,Mfupa mmoja wa mamba,ganda la moja la risasi pamoja na Ngozi ya nyoka.’’alisema Ngindo.
Aidha Ngindo amewataka wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo na hifadhina kufanya mauaji ya wanyama kwa lengo la kuondokana na matatizo yasiokuwa ya lazima.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.