Wananchi katika kijiji cha Matai asilia kata ya Matai wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wamejitolea kujenga vyumba vinne vya madarasa na kuiomba serikali kuwaunga mkono kwa kumalizia sehemu iliobakia kutokana na wao kufikia usawa wa lenta.
Wamesema mpaka kufikia hatua hiyo wametumia zaidi ya shilingi million arobaini na tano na kufanikiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofis moja na vingine viwili wakifikia usawa wa lenta.
Mwenyekiti kijiji hicho Pita Kaeke, amesema majengo yote yamejengwa kwa nguvu zao na kuelezea kuwa lengo ni kupunguza mlundikano wa wanafunzi katika shule ya msingi Matai ‘’A’’.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Emiliy Mwakalinga amesema serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi million 137,520,000,00 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa katika shule saba za msingi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.