JUKWAA la wanawake katika mikoa ya Rukwa na Katavi wameiomba serikali kutunga sheria mama ambayo itawawezesha kuwa na maamuzi katika jamii husani kushirikiana katika suala zima la mgawanyo na umiliki wa mali.
Ombi hilo waliliomba kupitia kikao kilicho keti hivi karibuni katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, na kuiomba serikali kufuta baadhi ya sheria za kimila ambazo zimekuwa kandamizi kwao na kuwanyanyasa katika jamii.
Walisema migogoro ya ardhi bado ni mingi na inasababisha wanawake wengi kupata matatizo hata pale ambapo makosa sio yao.
‘'kuna baadhi ya migogoro imekuwa ikisababishwa na mipaka,ufugaji wa kuhama hama, wawekezaji wakubwa na mfumo wa upimaji ardhi ,kwa hiyo tunaiomba serikali kuharakisha usuruhishi wa migogoro hiyo kwa wakati hususani maeneo ya vijijini'' Walisema.
Walisema ni vyema serikali ikajenga utaratibu wa kufanya kazi kwa kuweka ukaribu na mashirika yasio ya kiserikali na vikundi vya wanawake yanayojihusisha na haki za ardhi.
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo Elias Mtinda alisema wanawake waliowengi katika maeneo ya vijijini wanajishughulisha na kilimo na familia zao zimekuwa zikitegemea kupata mahitaji mengi kutoka mazingira yanayo wazunguka.
Alisema ukosefu wa huduma za ugani ,pembejeo za kilimo au mabadiliko ya tabia ya nchi ,imekuwa sababu kubwa ya wanawake kupata shida kwa kuwa wao ndiyo wanao wajibuka kwa asilimia mia katika katika jamii zao.
Alisema ili kumaliza tatizo hilo ni vyema serikali ikahakikisha utekelezaji wa bajeti ya kilimo inaongezwa pamoja na kuhakikisha asilimia ishirini ya makusanyo ya ndani ya halmashauri inarejeshwa kwa wakati sambamba na kuongeza maafisa ugani katika maeneo ya vijijijini.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika madhimisho hayo amewataka wanawake kujenga mazoea ya kujiunga na vikundi vya ujasiliamali ili kuwarahishisia kukopesheka.
Alisema malengo ya serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki sawa na kuwasihi viongizi kupitia idara ya maendeleo ya jamii kuhakikisha wanaatoa fedha asilimia kumi za wanawake na vijana ili kuyawezesha makundi hayo kunufaika zaidi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.