Wanufaika 1441 wa mradi wa kunusuru kaya masikini TASAF wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamehitimu kwenye mpango huo baada ya kufuzu kufuatia kufanyiwa tathimini na serikali baada ya kuwa kwenye mpango kwa kipindi cha miaka 9.
Wanufaika waliofuzu kwenye mpango huo ni wale waliotambuliwa kwenye mpango huo mwaka 2015 kutoka vijiji 66 vya wilaya hiyo na kubainika kuwa hawana sifa za kuendelea kunufaika kutokana na hali zao za kiuchumi kuimalika ukilinganisha na hapo awali.
Hata hivyo kwa kipindi cha kuanzia Januari 2025 wanufaika wapatao 6310 wameendelea kunufaika na mradi wa kunusuru kaya masikini (TASAF) wilayani humo ,ambapo kiasi cha shilingi million 189,983,080 kimetolewa kwa ajili ya wanufaika wanao pata fedha Taslimu na shilingi 33,851,867 ikiwa ni kwa ajili ya wanufaika 1080 wanao pata kwa njia ya mitandao ya simu na benki.
Taarifa kutoka idara ya maendeleo ya jamii imeeleza kuwa tathimini ya wanufaika wa mradi wa TASAF hufanywa kila baada ya miaka mitatu kupita na wanufaika wanao bainika hali zao za kiuchumi kuimarika huondolewa kwenye mpango huo kwa utaratibu maalum.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.