UONGOZI wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa umewaonya watendaji pamoja na wasimamizi wa uchaguzi utakao fanyika kesho kutojihusisha na vitendo vya udanganyifu vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Onyo hilo limetolewa jana na msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa wilayani hiyo Mbawala Kanoti katika kikao kazi kilicho fanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Alisema kuwa mara kwa mara wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vya kupigia kura ndiyo wamekuwa wakisababisha wananchi kutokuwa na imani na matokeo kutokana na baadhi yao kukiuka madili yao ya kazi kwa kuchukua hongo kutoka kwa wagombea.
Alisema kuwa kufanya kazi kinyume taratibu kumekuwa kukisababisha malalamiko hivyo kuwataka kujiepusha na vitendo hivyo ili kufanya uchaguzi huo kuwa wa amani.
"uzoefu unaonyesha sisi watendaji wa serikali ndio tumekuwa vinara kwani tumekuwatu kisababisha kuibuka malalamiko kutoka kwa wa pigakura ,pia lazima mkumbuke kuwa vyombo vya sheria havita wavumilia endapo mtakwenda kinyume na utaratibu'’alisema
Alisema kuwa katika uchaguzi huo vitongoji 78,vijiji 33 na kata 14, ndio vitashiriki katika uchaguzi huo.
Msimamizi huyo wa wilaya alisema kuwa katika wilaya hiyo jumla ya vijiji 78, vitongoji na kata 344 hakutakuwa na uchaguzi kutokana na wagombea wa baadhi ya vyama pinziani kujitoa na wengine kuondolewa kutokana na kuwekewa pingamizi hali inayotoa fursa kwa wagombea wa Chama cha Mapinduzi kupita bila kupingwa.
Alisema kuwa uchaguzi utaanza majira ya saa 2:00 za asubuhi na kuhitimishwa saa 10:00 za jioni na aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa lengo la kuchagua viongozi bora na ambao watakuwa masaada katika maeneo yao na taifa kwa ujumla.
Kwaupande wao watendaji pamoja na wasimamizi hao walisema kuwa wamejipanga vizuri ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na wanaimani kuwa hakutakuwa na malalamiko kwakua taratibu zote zitafuatwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.