Mkuu wa wilaya ya Kalambo Kalorius, Misungi amewataka watendaji kurejesha fedha za makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo kiasi cha shilingi million 162 na kusisitiza kuwakamata watendaji wote ambao watashindwa kurejesha fedha hizo ifikapo February 28 mwaka huu.
Agizo hilo alilitoa Jana kwenye Baraza la madiwani la halmashauri hiyo lililoketi jana kwaajili ya kupitisha mpango na bajeti ya matumizi ya mwaka wa fedha wa 2021/2022.
Alisema kuwa tangu Halmashauri hiyo ilipo anza utaratibu wa kukusanya mapato kwa mashine za kielektroniki na kuyapeleka Benki watendaji hao wamekuwa na tabia ya kutowasilisha fedha hizo Benki, na badala yake wamekuwa wakizitumia kwa matumizi yao binafsi
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa katika Halmashauri hiyo jumla ya watendaji 93 wamezitumia fedha kiasi cha shilingi 162,742,350 hivyo kuwataka wazirudishe kabla ya Februari 28 vinginevyo ataliagiza Jeshi la polisi kumkamata kila mtendaji anayedaiwa.
"Naagiza kuanzia leo hadi Februari 28, kila mmoja arudishe kiasi cha fedha anazodaiwa, ikipita tarehe hiyo nitampa orodha OCD inayo onesha kila mtendaji kiasi anacho daiwa na Kijiji alichopo na nitamuagiza amkamate ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake" alisema, Misungwi.
Mwenyekiti wa Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Daud Sichone, alisema kuwa Baraza hilo linaunga mkono agizo la mkuu wa wilaya kwani halipo tayari kuona watendaji wa serikali wanaongoza kuhujumu kodi za wananchi.
Alisema kuwa tangu mwaka 2017 kumekuwepo tabia ya watendaji kutumia fedha za makusanyo tofauti na maelekezo ya serikali hivyo ni lazima wazirudishe fedha hizo vinginevyo wengine hawatakuwa salama na watakwenda na maji kutokana na fedha hizo.
Licha ya hilo Halmashauri ya Kalambo kwa mwaka wa fedha 2021 /2022 inakadiria kukusanya, kupokea na kutumia jumla ya shilingi 34,416,806,430.00.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.