KATIBU tawala wilayani kalambo mkoani Rukwa Frank Schalwe amepiga malfuku viongozi wa serikali za vijiji na kata kuwatoza fedha kiasi cha shilingi elfu kumi {10000/=}wananchi pindi wanapopeleka malalamiko yao ofisini na kuisistiza kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watakao bainika kuendelea kufanya hivyo kutokana na fedha hizo kutozwa kinyume na utaratibu.
Kumekwepo na malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi juu ya viongozi wa serikali za vijiji kuwatoza wananchi fedha kiasi cha shilingi elfu kumi pindi wanapokuwa wakipeleka malalamiko yao kwenye ofis za vijiji na kata na hivyo kupelekea serikali wilayani humo kuitisha kikao cha pamoja kilicho jumuisha watendaji wa serikali za vijiji na kata, walimu wakuu, mafiasa tarafa pamoja na waratibu.
Awali akiongea na viongozi hao kupitia kikao kilichofanyika katika tarafa ya mwimbi , katibu tawala wilayani humo Frenk Schalwe amesema utozwaji wa fedha hiyo upo kinyume na utarabu.
‘’tumepata malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya watendaji kuhusika kwa namana mopja au nyingine kuwatoza fedha wananchi kuanzia elfu tano haadi elfu kumi kitu ambacho ni kosa kutokana na fedha hizo kuwa nje ya utaratibu ‘’alisema sichalwe.
Aidha amewasistiza viongozi hao kujenga mzoea ya kuwambia wananchi kupitia mikutano ya hadhara juu ya mafanikio ya serikali ya wamu ya tano ndani ya maeneo yao husiaka.
’’mesema kimsingi serikali imefanya mambo mengi hivyo kila kiongozi aliepo haapoa anapaswa juwa barozi kwa kuwambia wananchi yale mazuri ambayo serikali awamu yatano imekuwa ikifanya mfano imejenga vituo vine vya afya pamoja na hospitali ya wilaya hayo ni baadhi ya mambo mazuri ambayo serikali awamu ya tano inayatekeleza’’alisema schalwe.
Waratibu wilayani humo wameiomba serikali wilayani humo kuingilia kati swala la uendelezwaji wa makambi mashuleni kutokana na kukwamishwa na baadhi ya madiwani.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.