Watumishi wa umma wilayani kalambo mkoani Rukwa wametakiwa kufanya kazi kwa weredi na kwa kuzingatia miongozo ya serikali ikiwemo kujiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaweza kuhatarisha kazi yao.
Hayo yamebainishwa na afisa utumishi wilayani humo Amandus Mtani kupitia kikao cha mafunzo elekezi kwa watumishi wa ajira mpya wa kada tofauti ,ambapo amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 halmshauri ya Kalambo imepokea watumishi 102 wa ajira mpya wakiwemo walimu wa shule za msingi 61, sekondari 27,Afya 34, Biashara 1, Manunuzi 1,Mipango, 1, Takwimu 1, watendaji wa vijiji 10, Madereva 3 na Wasaidizi wa ofisi 3 na kuipongeza serikali kwa kutoa ajira hizo na kwamba zimesaidia kuondoa mapengo yaliokwepo awali.
Kwa upande wake mkuu wa Takukuru wilayani humo Lupakisyo mwakyolile aliwataka watumishi wa idara afya kujiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa na kusisitiza kufanya kazi kwa uadilifu ili kufikia malengo ya serikali.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.