Wazazi na walezi wilayani kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kuona uwezekano wa kuongeza idadi ya walimu wa madarasa ya awali ili kuendana na ongezeko la wanafunzi.
Hatua hiyo inakuja baada ya uwepo wa mwamko mkubwa wa wanafunzi wanao ripoti shule kwa mwaka 2024, ambapo hadi kufikia januari 26/2024 wanafunzi 12,017 kati yao wavulana wakiwa 5,766 na wasichana 6,25 sawa na asilimia 61 wameripoti shule idadi ambayo ni kubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Namlangwa Beni Mwanalinze,ambaye licha ya kuipongeza serikali kwa kukamilisha vyumba 39 vya madarasa ,alisema kuna haja ya walimu wa shule za msingi ikiwemo wa madarasa ya awali kuongezwa ili kuendana na ongezeko la wanafunzi wanao ripoti.
Aliko mkubwa mkazi wa kijiji cha Kalepula, alisema uwepo wa miundombinu rafiki ya shule imekuwa chanzo cha wanafunzi wa madarasa ya kwanza kuongezeka siku hadi siku na kusema serikali haina budi kuboresha vitendea kazi vya kujifunzia na kufundishia ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora kwa vitendo.
Awali akiongea wakati wa ukaguzi wa wanafunzi wanaoripoti kwenye shule mbalimbali wilayani humo, Kaimu afisa elimu msingi wilayani humo Kanuti Mbawala ,alisema hadi kufikia tarehe 18/1/2024 halmashauri ilikuwa na maoteo ya kuandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza 10,901 kati yao wavulana wakiwa 5,382 na wasichana 5,519 na kwamba hadi kufikia tarehe 18/1/2-26 halmashauri ilifanikiwa kuandikisha wanafunzi 9,492 kati yao wavulana wakiwa 4,771 na wasichana 4,721.
‘’Pia halmashauri tumefanikiwa kuandikisha wanafunzi wenye mahitaji maalumu 4 kati yao wavulana wakiwa ni 1 na wasichana wakiwa 3, ambapo hadi kufikia sasa halmashauri imefanikiwa kufikia asilimia 87 ya uandikishaji.’’alisema Kanuti.
Hivi karibuni akiongea kupitia mkutano wa waandishi wa habari, mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere, alisema serikali imekuwa na utaratibu wa kutoa ajira za kila mwaka na kwamba kwa mwaka 2024 serikali inatarajia kutoa ajira mpya ambazo zitawezesha kupunguza ikama ya wanafunzi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.