Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imeanza kutoa mafunzo kwa watendaji wa vijiji na wenyeviti wa serikali za viijiji juu ya matumizi sahihi ya mfumo mpya wa malipo ya serikali utakao wezesha kudhibiti matumizi mabaya ya fedha na kuweka uwazi wa matumizi ya fedha wakati wa utekelezaji miradi mbalimbali ya serikali.
Aidha mfumo huo utawawezesha wananchi kupata taarifa za mapato na matumizi kwa wakati kupitia mikutano ya hadhara ikiwa ni pamoja na halmashauri kujua mienendo ya michango ya wananchi itakayo kuwa ikiwasilishwa Benk kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Hata hivyo baadhi ya wenyeviti wa serikali za vijiji wameipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo huo na kwamba utawawezesha kuongeza ufanisi wa kazi na kuondoa usumbufu wa ufutiliaji wa fedha kwenye ofisi ya mkurugenzi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.