Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Tano Mwera amezindua Operesheni ya Anwani za Makazi katika Wilaya ya Kalambo kwa kuweka kibao cha Anwani ya Makazi katika jengo la Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kalambo leo tarehe 02, Machi 2022.
Wakati wa uzinduzi huo Mh. Mwera ameitaka timu inayotekeleza operesheni hiyo kufanya kazi kwa weredi na kwa haraka ili majengo yote katika Wilaya ya Kalambo yawe na Anwani za Makazi kufikia tarehe 28 Aprili 2022.
Aidha amewataka wadau mbalimbali zikiwepo taasisi za dini kusaidia kufikisha elimu katika jamii juu ya uwepo wa zoezi hili ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kutoka kwa wamiliki wa majengo katika Wilaya ya Kalambo. Mh. Mwera alisisitiza kuwa Operesheni ya Anwani za Makazi ni muhimu kuelekea katika Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 itakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu, hivyo ni lazima ikamilike kwa wakati.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.